tovuka.My Account ↗
Privacy · Updated 11 October 2026

Taarifa zako zinabaki kuwa muhimu.

Hii ni pilot privacy notice. Tovuka haipaswi kukusanya data zisizohitajika, kuuza customer information au kutoa private project information kwa mtu mwingine. Maelezo ya operator wa kisheria na data-protection registration yanahitaji kuthibitishwa kabla ya public commercial rollout.

1. Tunakusanya taarifa zipi?

Tunaweza kupokea jina la biashara, maelezo ya huduma/bidhaa, jina la mwenye biashara, email, WhatsApp, location ya biashara, logo, picha na maoni ya website. Wateja wanaotuma enquiry wanaweza kutoa jina, simu, aina ya order/booking, tarehe wanayopendelea na maelezo. Malipo ya Tovuka yanaweza kuhusisha transaction reference na proof ya verification. Hatuombi password au OTP ya malipo.

2. Kwa nini tunatumia data?

Kutengeneza na kuhudumia website yako, kuonyesha taarifa ulizoruhusu ziwe public, kukupatia status, kushughulikia enquiries, kuhakiki malipo, kupokea support requests na kulinda mfumo dhidi ya matumizi mabaya. Marketing emails zinahitaji opt-in pale sheria inapotaka.

3. Nani anaweza kuona data?

Staff walioidhinishwa wanaweza kushughulikia project, malipo na support kwa kazi zao. Mmiliki wa biashara anaweza kuona requests za website yake kupitia authenticated dashboard. Public visitors wataona taarifa za website zilizochapishwa tu. Infrastructure providers wanaweza kuchakata data kwa ajili ya hosting, storage na email delivery, ikiwa ni pamoja na Cloudflare na Supabase, kulingana na mikataba na mipangilio yao.

4. Storage, transfers & retention

Website na account information zinaweza kuhifadhiwa au kuchakatwa kwenye miundombinu ya cloud ambayo inaweza kuwa nje ya Tanzania. Tunaweka access controls na tunapunguza exposure ya taarifa. Tutatoa retention periods zilizoainishwa kwenye final policy. Unaweza kuomba access, correction au deletion kulingana na sheria inayotumika na record-keeping obligations.

5. Customer website enquiries

Mteja wa Tovuka anamiliki wajibu wa kutunza data za wateja wake na kutumia data kwa madhumuni aliyowajulisha. Kwa huduma maalum, majukumu ya data controller na processor yatafafanuliwa kwenye mkataba. Usitume data nyeti kwenye free-text enquiry forms.

6. Cookies & analytics

Tunatumia session/authentication mechanisms na basic page-view counting. Hatutadai kwamba hakuna third-party processing. Marketing tracking/cookies za ziada zinahitaji notice/consent zinazofaa kabla ya kuwashwa.

7. Usalama & taarifa za ukiukaji

Tunatumia project isolation, restricted staff access na SSL/TLS ya hosting platform. Hakuna website iliyo na zero risk. Tutachunguza security incidents na kutoa taarifa zinazotakiwa chini ya sheria inayotumika.

8. Mawasiliano

Kwa privacy questions, correction au deletion requests: teamtovuka@gmail.com. Tafadhali toa business/project reference, si password au OTP.